17 Machi 2023 - 21:58
Putin: Ujerumani bado iko chini ya uvamizi wa Marekani

Rais wa Russia amesema kuwa nchi za Ulaya hazina ujasiri wa kutoa maoni kuhusu milipuko iliyotokea kwenye mabomba ya kusafirisha gesi ya Nord Stream kutokana na kutokuwa huru.

Akizunguzma katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Russia-1, Rais Vladimir Putin amesema kwamba jibu la Ujerumani kwa milipuko ya mabomba ya gesi ya Russia limethibitisha kuwa nchi hiyo bado inakaliwa kwa mabavu, miongo kadhaa baada ya kumalizika Vita vya Pili vya Dunia. 

Putin ameongeza kuwa, Umoja wa Kisovieti uliondoa vikosi vyake kutoka Ujerumani na kukomesha kuikalia kwa mabavu nchi hiyo; Lakini kama inavyowazi, hali haikuwa hivyo kwa Wamarekani kwa sababu bado wanaikalia kwa mabavu Ujerumani.

Tarehe 27 Septemba, 2022, kuliripotiwa uharibifu mkubwa kwenye mabomba ya Nord Stream, na wataalamu wa matetemeko ya ardhi wa Uswidi walirekodi milipuko miwili mnamo Septemba 26 kando ya njia za mabomba hayo. Kulipuliwa kwa mabomba ya Nord Stream 1 na 2 kulishusha chini usafirishaji wa gesi na kuvuja kwa bidhaa hiyo katika Bahari ya Baltic.

Mwakilishi wa Kudumu wa Shirikisho la Russia katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzya amesema kuwa milipuko iliyotokea kwenye mabomba ya gesi ya Nord Stream 1 na Nord Stream 2 ni ugaidi wa kimataifa.

Mnamo siku ya Jumatano ya tarehe 8 Februari, ripota mchunguzi wa Marekani, Seymour Hersh, alitoa ripoti yake ya uchunguzi aliofanya, akiishutumu serikali ya Washington kuwa ndiyo iliyohusika na miripuko iliyotokea Septemba mwaka jana kwenye mabomba ya usafirishaji gesi ya Nord Stream. 

Nord Stream

Kulingana na chanzo cha habari cha kuaminika kilichozungumza na Hersh, mada za miripuko ziliwekwa kwenye mabomba makuu katika Bahari ya Baltic mnamo Juni 2022 na wazamiaji wa Jeshi la Marekani kwa kutumia kivuli cha mazoezi ya kijeshi ya shirika la NATO na kisha yakaripuliwa baadaye kwa kutumia rimoti kutokea mbali.

342/